Lugha: Kiswahili | Kiingereza | Kinorwei

Tangu 1.1.2015 kazi ya vitabu vya Scripture Mission viliungana na shirika la Soma Biblia. Muunganiko imetusaidia kuongeza biashara na kazi ya kuchapisha. Kusoma zaidi juu ya Soma Biblia, ingia kwenye website yetu www.somabiblia.or.tz

Karibu Scripture Mission
Hata hivyo, mahali pa Scripture Mission Arusha, panaendelea kusaidia kazi ya fasihi kwa njia ya kukodisha nafasi ya ofisi ya Soma Biblia Publishing Department. 


Duka la vitabu limehamia mjini. Mawasiliano na ramani ya duka, inapatikana hapa: http://www.somabiblia.or.tz/arusha/

Pia, katika mahali pa Scripture Mission tuko na nyumba ya wageni. Tuna vyumba vinne, jikoni na sebuleni. Nyumba ya wageni ni mwanzoni kwa ajili ya wafanyakazi wa shirika la NLM, DLM na SMEA. Lakini kama tunanafasi, wengine wanaweza kukodisha. 
Kuomba chumba, tuma barua pepe kwa: nlmear.arusha@nlm.no 
Au mpigie simu Station Manager yetu, Joakim Ami: +255 784 590 870.

Ofisi ya MAF, Hamasa ya Milele,
Scripture Mission na Soma BibliaKatika Scripture Mission unatafuta pia:
Ofisi ya MAF Tanzania
Ofisi ya FIDA international Tanzania
Ofisi ya Hamasa ya Milele TanzaniaIngawa inaweza kuonekana kuwachanganya kidogo, lengo la Scripture Mission na majengo yote hapo, ni kushirikiana katika maono "Ulimwengu kwa Kristo"!


Karibu! Welcome! Velkommen!

– Tunaposhindwa kuwahubiria watu Neno la Mungu tunakuwa wachoyo na kutawaliwa na ubinafsi, anasema Mchungaji Christopher Mbuga katika toleo la mwisho la Riziki.

Askofu mlutheri alipoulizwa kama missioni ni muhimu kwa kanisa, alijibu: «Kanisa NI missioni». Yaani, kanisa ambalo halifanyi kazi ya missioni, siyo kanisa hai.

Toleo la kwanza ya 2013 linahusu uinjilisti kwa jirani. Tena tunatoa mfano kutoka dayosisi ya Mbulu: Wadatooga waliachwa wakati KKKT kanisa la Mbulu lilipoanza. Lakini siku hizi kanisa limeona wajibu wake wa kuhubiri Injili kwa jirani zao wadatooga, nao wameanza kutoa sifa zao kwa Yesu.


Upate nakala yako kutoka kwa Scripture Mission:
Barua pepe: arusha@scripture-mission.com 
Simu: +255 787 312 369

Toleo la tatu la Riziki 2012 linahusu ulevi.

Usome kuhusu mwinjilisti aliyekuwa mlevi mwenyewe, na anayetumia muda wake kushuhudia watu wengine.

Haydom Lutheran Hospital katika Mbulu wanatoa matibabu kwa wagonjwa wa ulevi.
– Yeye mwenyewe anahitaji kuona kwamba ana shida ya ulevi na kuridhia. Ulevi ni ugonjwa lakini matibabu yapo, anasema Paulo Tango, kiongozi wa Amani Wodi.

Upate nakala yako kutoka Scripture Mission Arusha.

Toleo la pili la Riziki 2012 linahusu waislamu. Hatujaitwa kuwabadili dini yao, tumeitwa kuhibiri Injili.

– Kabla ya kwenda kumpelekea Injili Mwislamu awaye yote, jipime mwenyewe. Je, unampenda huyo Mwislamu?

Upate nakala yako kutoka Scripture Mission Arusha.

Je, viongozi wanyenyekevu wameisha? Kama heshima ya Wachungaji imepanda juu mpaka watu wanamwogopa Mchungaji, tumepotea.

Yesu alitupa kielelezo kizuri sana alipowatawadha miguu. Anayetaka kuwa mkubwa awe mtumishi, tumesikia kanisani. Tunatekelezaje? Tuwe vielelezo kwa waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Usome Riziki toleo la kwanza 2012.

Hujapata bado? Tuma barua pepe kwa arusha@scripture-mission.com 

Utupigie ukitaka toleo la mwisho la Riziki:
Kanisa bila udiakonia halina uhaiKaribuni kututembelea kwenye duka jipya! Limetengenezwa vizuri na wafanyakazi wetu; Sebastian na Ole Andre. Karibuni kuona na kuzoea duka lililoboresha :)